Hofu ya Borno kutekwa na Boko Haram

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanamgambo wa Boko Haram wanatumia silaha nzito kama hizi kupambana na jeshi

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan anafanya kikao cha dharura cha ulinzi mjini Abuja huku ripoti zikisema kuwa huenda jimbo lililo Kaskazini mashariki la Borno likaingia mikononi mwa kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Vyombo vya habari vinasema kuwa viongozi saba wa kitamaduni wametoroka makwao.

Siku ya jumamne kundi la Boko Haram liliuthibiti mji wa Bama ambao ni mji wa pili kwa ukubwa kwenye jimbo la Borno ambapo liwaua watu wengi na kuwalazimu maelfu ya wengine kukimbia makwao .

Kwa sasa ni mji mkuu tu wa jimbo la Borno wa Maduguri ulio chini ya udhibiti wa vikosi vya serikali.