Rais Obama alaani mauaji ya mwandishi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwandishi Mmarekani Steven Sotloff aliyeuawa kwa kunyongwa na wapiganaji wa kiisilamu

Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Marekani haitatishwa na mauaji wa mwandishi mwingine wa habari Mmarekani na kundi la Islamic state.

Akiongea na waandishi wa habari nchini Astonia Rais obama amesema kuwa mauaji hayo yanaichochea Marekani kukabiliana ziani na magaidi

Mapema Marekani ilisema kuwa kanda ya video inayoonyesha kuchinjwa kwa mwandishi huyo Steven Sotloff ni ya ukweli

Video hiyo iliyotolewa na kundi la wanamgambo wa Islamic State inamuonyesha mwanamme aliyejifunika uso wake na kisu mkononi akisimama juu ya Sotlof.

Nchini uingereza waziri mkuu David Cameron ameongoza mkutano wa kamati ya dharura ya serikali kujalidili jinsi itakavyojibu tishio la kutaka kumuua mateka raia wa uingereza.

Kwenye video hiyo mwanamgambo aliyejifunika uso na anayezungumza kiingereza anayaonya mataifa ya kigeni na kuyataka kusitisha harakati zao dhidi ya kundi la Islamic State.

Sotlof ni mwandishi wa pili wa Mmarekani kuuawa kwa kukatwa kichwa ndani ya mwezi mmoja baada ya mwandishi mwingine James Foly kuuawa kwa kukatwa kichwa mwezi uliopota na wanamgambo wa ISIS.