Mafuriko yaua nchini India

Image caption Mafuriko Kashmir, India

Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuchukuliwa na maji katika jimbo la Kashmir nchini India. Basi hilo lilikuwa limebeba abiria hamsini walitoka katika sherehe za harusi wakiwemo bibi na bwana harusi.

Ofisa wa polisi katika eneo la Kashmir Owais Ahmad ameiambia BBC kuwa mafuriko yanazidi kuongezeka na jitihada za uokoaji zinaendelea. Eneo hilo limekumbwa na mafuriko makubwa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 22, ambapo watu tisa wamepoteza maisha tangu mafuriko hayo yatokee Jumanne. Ajali za barabarani nchini India zimekuwa zikitokea mara kwa mara ambapo takwimu za serikali zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 138,000 walikufa mwaka jana, 2013 kutokana na ajali hizo.