Al-Qaeda yafungua tawi jipya India

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption kiongozi wa Al-Qaeda Aymal al-Zawahiri

Kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri amesema kuwa wamefungua tawi jipya la mtandao huo wa kigaidi nchini India ikiwa ni jitihada za kuhakikisha wanapandisha bendera za Jihad kusini mwa bara la Asia.

Taarifa zinasema kuwa picha za video za tangazo hilo zinasema kuwa hiyo ni hatua ya kuimarisha dola ya Kiislam ambao kwa sasa unashikilia eneo kubwa la Iraq na Syria.

Zawahiri amesema kuwa nguvu mpya ya mtandao inalenga kuvunja mipaka ya nchi na kuunganisha ukanda wa dola ya Kiislam kwa kuendesha mapigano kutoka India hadi Burma.

Hata jitihada za kundi hilo kutaka kuongeza himaya ya dola ya kiislam kusini mwa bara la Asia.