Watoto milioni 120 wafanyiwa ukatili duniani

Haki miliki ya picha twitter
Image caption Mtoto akijilia nyama

Umoja wa mataifa umetoa kauli kwamba wasichana zaidi ya milioni 120 duniani kote,sawa na msichana mmoja kati ya kumi atakua amaebakwa ama amewahi kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kabla hajatimiza umri wa miaka 20.

Kitengo cha umoja wa mataifa kinachoshughulikia masuala ya watoto UNICEF kimegundua mnamo mwaka 2012 pekee watoto na mabinti wapatao elfu tisini na watano waliuawa,wengi wao ni kutoka Marekani kusini na Caribbean.

Ripoti hiyo ya UNICEF iliangazia nchi zipatazo mia moja na tisini, na kusema kwamba duniani kote watoto wametendewa ukatili,mauaji na mashambulizi ya kingono ikiwemo kuonewa na uadabishaji watoto unaokiuka haki zao.