Watu 36 wafariki katika ajali Tanzania

Takriban Watu 36 wamefariki na wengine 79 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu, mabasi mawili na gari dogo ajali iliyotokea Mkoani Mara, Kaskazini mwa Tanzania.

Eneo hasa ambako ajali hiyo ilitokea ni katika barabara ya Musoma- Mwanza mabasi hayo yaligongana uso kwa uso katika eneo la Saba Saba wilaya ya Butiama mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Alex Karangi ameiambia BBC kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa tano asubuhi katika eneo la sabasaba

Kamanda Karangi amesema Kabla ya kugongana uso kwa uso kwa mabasi hayo , gari dogo liligongwa na basi lililokuwa likitoka mkoani mwanza na kutumbukia mtoni.

Uchunguzi unafanyika kubaini chanzo cha ajali hiyo na hivi sasa majeruhi wako hospitali ya mkoa wilayani Musoma.

Utaratibu wa kuwatambua waliopoteza maisha katika ajali hiyo unaendelea.