Mkataba wafikiwa kusitisha vita Ukraine

Haki miliki ya picha AFP

Serikali ya Ukraine na wapiganaji wa nchi hiyo wanaounga mkono Urusi wamekubaliana kusitisha mapigano yaliyodumu miezi kadhaa mashariki ya nchi hiyo.

Makubaliano hayo,yalifikiwa katika mazungumzo kati ya pande hizo mbili pamoja na wajumbe katika eneo la Minsk.

Kiongozi wa Ukraine, Petro Poroshenko, anasema kuwa kwa sasa ni muhimu kwamba mkataba huo wa mazungumzo utadumu.

Akiongea katika mkutano viongozi wa NATO, unaoendelea Wales, Rais Poroshenko, amesema kuwa hatua ya kubadilishana kwa wafungwa inapaswa kufanyika hivi punde.

Mapigano yamekuwa yakiendelea nchini Ukrainekwa siku nzima leo karibu na eneo mji unaodhibitiwa na serikali wa Mariupol.

Wakati huohuo, Marekani na muungano wa ulaya zinapanga kutangaza vikwazo zaidi dhidi ya urusi licha makubaliano ya kusitisha mapigano yataafikiwa hii leo mjini Belarus.

Waziri wa masuala ya kigeni wa uingereza Phlip Hammond ambaye anahudhuria mkutano wa jumuiya ya kujihami ya NATO amesema kuwa watandelea na vikwazo zaidi akisema kuwa nchi za magharibi hazitaachana na shinikizo dhidi ya Rais wa Urusi.

Lakini amesma kuwa vikwazo hivyo vitaondolewa ikiwa usitishwaji mapigano utatekelezwa