USA:hatutashirikiana na Iran nchini Iraq

Haki miliki ya picha iran
Image caption Kiongozi wa dini Iran Ayatollah Ali Khamenei

Marekani imesema kuwa haina mpango wa kushirikiana na Iran kukabiliana na wapiganaji wa Islamic State waliopo nchini Syria na Iraq.

Msemaji wa idara ya Ulinzi nchini humo amesema kuwa Marekani pia haitabadilishana taarifa za kijasusi na Iran.

Taarifa hiyo ilitolewa baada ya duru za Iran kuiambia BBC kwamba kiongozi mkuu wa dini nchini humo Ayatollah Ali Khamenei alimuagiza kamanda mmoja wa jeshi la taifa hilo kusaidia katika oparesheni za kuwakabilia wapiganaji hao wa Islamic state kazkazini mwa Iraq akishirikiana na marekani,serikali ya Iraq na vikosi vya kikurdi.

Hatahivyo idara ya maswala ya kigeni nchini Iraq imekana mada hayo.