Morsi ashtakiwa kwa kutoa siri za Misri

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mohammed Morsi akiwa Kizimbani

Kiongozi mkuu wa mashtaka nchini Misri amemfungulia mashtaka aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi kwa kupeleka stakhabadhi za siri kutoka idara ya usalama nchini Qatar.

Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa jela tangu jeshi limuondoe madarakani mwaka uliopita wakati wa maandamano ya kumtaka ajiuzulu.

Tayari kiongozi huyo anakabiliwa na hukumu ya kifo katika mahakama nyengine tofauti.

Kundi la Muslim Brotherhood ambalo ni mwanachama wa maisha limepigwa marufuku na viongozi wake wengi huku wengine wakihukumiwa kifo.

Qatar imekuwa ikimuunga mkono Bwana Morsi .