Makubaliano ya amani yaheshimiwa Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkutano mgogoro wa UKraine mjini Misk

Baada ya miezi kadhaa ya mapigano nchini Ukraine,Serikali na waasi wanaounga mkono Urusi wamekubaliana kusitisha vita.

Makubaliano hayo yaliafikiwa kati ya pande pinzani pamoja na ujumbe wa Urusi katika mji wa Misk ambao ndio mji mkuu wa Belarus.

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema kuwa ni muhimu kwamba kuna mazungumzo kuhusu suluhu ya kisiasa.

Lakini waasi hao wamesema kuwa makubaliano hayo hayajabadilisha mpango wao wa kutaka kujitenga na Ukraine.

Mwandishi wa BBC katika mji wa ukraine Donetsk amesema kuwa hakuna vita vilivyo ripotiwa tangu makubaliano hayo yatangazwe.