Watu saba wahukumiwa kifo kwa ubakaji.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa genge la washukiwa wa ubakaji nchini Afghanistan

Watu saba wamehukumiwa kifo baada ya kuwabaka kwa zamu wanawake wanne nje ya mji mkuu wa Afghanista,kabul mwezi uliopita.

Hukumu hiyo inajiri baada ya kesi iliochukuwa masaa mawili na nusu ambapo wawili kati ya saba hao walikana madai hayo.

Mwathiriwa mmoja ilibidi alazwe hospitalini kufuatia kitendo hicho huku mwengine akidaiwa kuwa mja mzito.

Hukumu hiyo ya kifo ilitolewa kwa kosa la wizi wa mabavu huku hukumu ya miaka kumi na tano ikisimamia ubakaji.

Rais Hamid Karzai aliunga mkono wito wa watu hao kunyongwa hadharani iwapo watapatikana na makosa.