Iraq:Marekani yawashambulia wana Jihad

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Makabiliano nchini Iraq

Marekani imetekeleza mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Islamic State karibu na bwawa la Hadatha magharibi mwa Iraq.

Ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa Marekani kuendeleza mashambulizi yao ya angani hadi katika mkoa wa madhehebu ya kisunni wa Anbar.

Maafisa wa Marekani wamesema kuwa mashambulizi hayo manne ni ya kuwaunga mkono wanajeshi wa Iraq ambao wanalidhibiti bwawa la hadatha lililopo mto Euphrates.

Waziri wa ulinzi nchini humo Chuck Hagel amekana madai kwamba mashambulizi hayo ni ongezeko la ushirika wa Marekani nchini Iraq,akisema kuwa bwawa la Hadatha ni kiungo muhimu cha Iraq na kwamba maslahi ya Marekani yatatishiwa iwapo bwawa hilo litatekwa.