Boko Haram wauteka mji mwingine

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mamia ya watu wametoroka makwao kufuatia vita kati ya wapiganaji hao na jeshi

Kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Nigeria Boko Haram, wameuteka mji mwingine Kaskazini Mashariki ya nchi hiyo.

Mji huo Michika ulio katika jimbo la Adamawa, ilitekwa siku ya Jumapili , siku mbili baada ya mji jirani wa Gulak kutekwa na wapiganaji hao.

Wakazi wa Michika waliotoroka vita walisema walipigwa na mshtuko na kulazimika kutoroka kwani wapiganaji walikuwa wanapiga risasi watu kuholea walipowasili katika magari yao.

Walioshuhudia mapigano hayo walisema kuwa wapiganaji hao walijificha ndani ya nyumba za wakazi waliokuwa wametoroka vita pale ndege ya kijeshi ilipokuwa inazunguka eneo hilo kuwatafiuta wapiganaji hao.

Jeshi la Nigeria, limesema kuwa lilifanikiwa kuwaua wapiganaji 50 wa Bokjo Haram, katika makabiliano makali katika jimbo la Borno.