Marekani kusaidia kupambana na Ebola

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais Barack Obama wa Marekani

Serikali ya Marekani imeahidi kusaidia mapambano dhidi ya Ebola.

Rais Barack Obama amesema nchi yake itapeleka vifaa vyake vya kijeshi ili kusaidia kupambana na ugonjwa huo uliozuka katika nchi za Afrika Magharibi.

Akizungumza katika kipindi cha televisheni ya NBC, nchini Marekani, Rais Obama amesema iwapo dunia haitachukua hatua za haraka, ugonjwa wa ebola utaweza kusambaa nje ya Afrika na kutishia usalama wa nchi yake.