Watawa 3 maajuza wauawa Burundi

Haki miliki ya picha reuters
Image caption Maafisa wa kanisa wanasema kuwa watawa hao waliuawa na mhali mwenye akili pungwani

Watawa watatu wakongwe wamebakwa na kuuawa mjini Bunjumbura katika makazi ya watawa wanawake viungani mwa mji mkuu huo.

Sababu ya mauaji hayo haijulikani. Polisi wanasema kuwa wamewazuilia washukiwa wawili, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Watawa hao walisemekana kuwa Lucia Pulici,mwenye umri wa miaka 75, Olga Raschietti, 82 na Bernadetta Boggian, 79.

Wawili kati ya waathiriwa, waliuawa Jumapili huku mwili wa mwingine wa tatu ukipatikana Jumatatu ukiwa umekatwakatwa.

Maafisa wakuu wanasema kuwa mshukiwa wa mauaji hayo, alionekana akitoroka makazi ya watawa hayo akiwa ameshika kisu mkononi

Dayosisi ya Italia ya Parma inasema kuwa watawa hao waliuawa wakati wa jaribio la wizi katika makazi yao.

Hata hivyo haijulikani kwa nini watawa hao waliuawa kwani hakuna kilichoibwa kutoka kwao.

Haki miliki ya picha
Image caption Ramani ya Burundi

Kwenye mtandao wake, dayosisi ya kikatoliki ya Parma ilisema kuwa mauaji ya watatu hao yalifanywa na mhalifu ambaye alikuwa na matatizo ya kiakili.

Watawa hao wawili walikuwa wanashiriki katika kanisa katoliki la Xaverian.

Mnamo mwaka 2011,mtawa mmoja na mfanyakazi wa shirika la misaada aliuawa katika tukio la ujambazi Kaskazini ya Burundi

Burundi ni moja ya nchi masikini ambapo uchumi wake unategemea sana mapato kutokana na Chai na Kahawa zinazouzwa nje.