Bunge la Iraq laidhinisha serikali mpya

Haki miliki ya picha NA
Image caption Wabunge wa Iraq

Bunge la Iraq limeidhinisha serikali mpya itakayoshirikisha makundi muhimu nchini humo.

Serikali hiyo inaongozwa na Waziri Mkuu Haidar al Abadi, huenda ikasababisha nchi hiyo kuondokana na makundi ya wapiganaji wanaotishia usalama wa nchi, endapo kutakuwa na kuaminiana miongoni mwa wananchi.

Hata hivyo hakuna Waziri wa ulinzi wala wa mambo ya ndani ya nchi aliyetangazwa mpaka sasa.

Lakini Waziri mkuu wa nchi hiyo amesema atafanya uteuzi wa mawaziri hao kwa muda wa wiki moja.

Nafasi nyingine za mawaziri zimejazwa kwa mujibu wa makubaliano kati ya Washia walio wengi, Wasunni na Wakurd.

Serikali hiyo imeonekana ni muhimu katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa kundi la Islamic State.