Ndege ya MH17 ya Malaysia ilidunguliwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Muombolezaji akiweka saini kama ishara ya kutoa pole zake kwa waathiriwa

Wachunguzi wa Uholanzi waliokuwa wanachunguza chanzo cha ajali ya ndege ya Malaysia nchini Ukraine mwezi Julai wanasema kuwa ndege hiyo ya abiria ilikumbwa na kitu chenye ncha na kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye mionzi mikali.

Mwandishi wa BBC amesema kwamba ushahidi huo ni wa wazi na kwamba ndege hiyo ilishambuliwa kwa kombora.

Katika ripoti yao ya kwanza ya kiuchunguzi ,maafisa hao wa Uholanzi wanaojihussha na masuala ya usalama wa anga wameeleza kua hapakuwa na tatizo la kiufundi lililosababisha ndege hiyo ipate ajali, ama makosa ya rubani yalosababisha ndege hiyo kulipuka.

Wataalam hao wameendelea kueleza kwamba kisanduku cha kurekodia mwenendo wa ndege hiyo hakikuonesha kwamba kulikua na dharura.

Abiria wote miambili na tisini na nane walipoteza uhai pindi ilipoanza safari kutoka uwanja wa ndege wa Amsterdam kueleke Kuala Lumpur.Kutokana na ajali hiyo kuna shaka kwamba vikundi vya waasi wa Urusi viliiidungua ndege hiyo.

Lakini mpaka sasa Urusi imepinga kuhusika kwa namna yoyote na ajali hiyo.

Inaarifiwa kwamba ripoti kamili juu ya ndege hiyo MH17 itatolewa mwakani.