Meya mwenye utata alazwa hospitalini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meya Rob Ford amewahi kukiri kutumia dawa za kulevya

Meya wa Toronto, anaekumbwa na utata Rob Ford, amelazwa hospitalini baada ya kupataikana na uvimbe tumboni mwake.

Alikwenda hospitalini akiwa na maumivu makali ya tumbo. Madaktari hawajaeleza uzito wa tatizo hilo la kiafya la Meya huyo hadi wafanye uchunguzi zaidi.

Bw. Ford, aligonga vyombo vya habari mwaka jana pale alipokiri kutumia mihadarati aina ya cocaine na kuwa anakabiliwa na tatizo la ulevi.

Awali kipindi cha miezi miwili alitafuta usaidizi wa kitabibu kujaribu kuacha uraibu wa kutumia dawa za kulevya na pombe na Alirudi ofisini hapo Juni.

Licha ya hayo amejitosa kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mwezi ujao akitafuta muhula mwengine kama meya.