Marekani kupambana na Islamic State

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Marekani Barack Obama

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa tamko kua hatasita kuchukua hatua stahiki dhidi ya kikundi cha wanamgambo wa dola ya kiislam huko Syria na Iraq.

Katika hotuba yake kwa taifa hilo ilooneshwa kupitia runinga ya taifa ameelezea mipango yake ya utekelezaji dhidi ya wanamgambo hao kua kikundi chochote cha kigaidi kitakachoitishia Marekani hakitakua salama milele.

Rais Obama pia amesema kwamba kikosi namba 475 watapelekwa Iraq ingawa hawatakua na jukumu lolote la kupambana na wanamgambo hao.

Inaelezwa kuwa kundi hilo la wanamgambo wa dola ya kiislam wanatwala eneo kubwa la Syria na Iraq,na wanamgambo hao wamegeuka kua hatari kwa matendo yao ya kuua watu kwa kuwakata vichwa waandishi wa habari kutoka ughaibuni huku ulimwengu ukishuhudi.

Marekani imesha fanya mashambulizi ya anga yapatayo

150 dhidi ya kikundi hicho cha Is na kugawanya silaha kwa wale wanakipinga kikundi hicho Iraqi vikundi vya ki Kurdi .

Katika hotuba yake hiyo ilodumu kwa muda wa dakika rais huyo amesema huu ni muda muafaka Marekani kuingilia kati na lazima Marekani itaongoza na kuwarejesha nyuma wanamgambo hao wa IS.

Akiizungumzia Iraq, amesema ataongeza nguvu za kulinda raia wa Marekani na kusambaza misaada ya kibinaadamu na tutaipiga Is .

Rais Obama amesema kwamba anakaribisha uungwaji mkono kutoka katika Bunge la Marekani lakini kwa mamlaka laonayo anayweza kuendelea na dhamira yake bila ruhusa ya bunge hilo.

Rais Obama alichaguliwa na chama chake cha Democrat kwasababu ya ari yake ya kupinga uvamizi katika nchi ya Iraq mnamo mwaka 2003 na kuongoza harakati za kuondoa wanajeshi wa Marekani nchini humo.