Marekani yatinga fainali kikapu

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kombe la dunia mpira wa kikapu

Marekani yatinga fainali kombe la dunia mpira wa kikapu kwa kuiangushia kichapo Lithuania.

fainali za kombe la dunia la mpira wa kikapu zinazoendelea huko nchini Hispania ikiwa Marekani tayari imetinga fainali hizo kwa kuifunga Lithuania vikapu 96 kwa 68, na hivyo inaisubiri moja wapo kati ya Ufaransa na Serbia zitakazopambana baadaye leo.

Lithuania inamsubiri atakayopoteza katika mechi hiyo ili kutafuta mshindi wa tatu kesho huku fainali yenyewe ikisubiriwa jumapili.