Jengo laporomoka na kuwaua watu Nigeria

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Jengo lililoporomoka

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki mjini Lagos Nigeria baada ya jengo moja linalohusishwa na muhubiri mashuhuri nchini humo TB Joshua kuanguka.

Ripoti zinasema kuwa miili kadhaa imetolewa katika vifusi vya jengo hilo.

Shirika la kusimamia dharura nchini humo NEMA ,limesema kuwa jengo hilo ni la nyumba za kulala za wanachama wa kanisa la All Nations katika wilaya ya Ikotun.

Jengo hilo la ghorofa mbili lilikuwa likiongezwa ghorofa nyengine mbili lilipoanguka.

Maelfu ya watu mara nyingi uhudhuria maombi yanayoongozwa na TB Joshua anayejulikana kama mtume,kwa kuwa wanavutiwa na uwezo wake wa kuwaponya watu.