Maafisa 10 wakataa kurudi nchini Liberia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Sirleaf Johnson wa Liberia

Rais wa Liberia Sirleaf Johnson amewafuta kazi maafisa kumi wa serikali kwa kukataa kurudi nchini humo wakati ambapo taifa hilo linakabiliana na maambukizi hatari ya ugonjwa wa Ebola.

Maafisa hao waliagizwa kurudi nchini humo mwezi mmoja uliopita.

Rais Sirleaf amewashtumu kwa kutojali janga linalowakumba raia wa taifa hilo.

Bi Sirleaf ameripotiwa kuomba msaada zaidi kwa serikali ya rais Obama ili kukabiliana na virusi hivyo.

Ameitaka Marekani kujenga kituo kimoja cha kuwatibu wagonjwa wa Ebola katika mji mkuu wa Monrovia.

Virusi hivyo vimewaua zaidi ya watu 2,400 Magharibi mwa Afrika tangu mwezi Machi ,nusu ya raia hao wakitoka nchini Liberia.