Je,Scotland itajitenga na Uingereza?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wa Scotland

Huku pande pinzani kuhusu kura ya maamuzi nchini Scotland zikiimarisha juhudi zao za kutaka kuungwa mkono kabla ya kufanyika kwa shughuli hiyo siku ya alhamisi,matokeo ya kura mpya ya maoni yanaonyesha kuwa upande wowote unaweza kuibuka mshindi.

Kura nyengine nne za maoni zimechapishwa mwishoni mwa juma hili huku tatu kati yake zikionyesha ushindi mdogo kwa wale wanapinga kujitenga.

Mwandishi wa BBC anayesimamia maswala ya kisiasa amesema kuwa wapiga kura ambao bado hawajaamua huenda wakawa muhimu.

Maelfu ya wanaharakati wanatarajiwa kufanya maandamano katika barabara za miji ya Scotland hii leo ili kutafuta kuungwa mkono.