Uganda yatibua shambulizi la kigaidi

Image caption Vikosi vya usalama nchini Uganda

Maafisa wa polisi nchini Uganda wameimarisha usalama katika maeneo mengi ya uma katika mji mkuu wa Kampala kufuatia kukamatwa kwa washukiwa kadhaa wa makundi ya kigaidi na vilipuzi.

Msemaji wa polisi ameiambia BBC kwamba jaribio la kutekeleza mashambulizi limetibuliwa.

Awali ,ubalozi wa Marekani mjini Kampala ulisema kuwa mamlaka ilitibua shambulizi la kigaidi lilokuwa limepangwa na washukiwa wa kundi la Alshabaab.

Ubalozi wa Marekani umewataka raia wake nchini Uganda kuendelea kukaa majumbani mwao.

Ubalozi huo tayari ulikuwa umeonya kuhusu shambulizi la kulipiza kisasi dhidi ya maeneo ya Marekani na kundi la Alshabaab ili kujibu shambulizi la angani la Marekani lililomuua kiongozi wa kundi hilo mapema mwezi huu.