Mnara mrefu zaidi katika msitu wa Amazon

Image caption Mnara wa kimo kirefu zaidi duniani kujengwa katika msitu wa Amazon

Nchi ya Brazil imeanza rasmi ujenzi wa mnara mrefu zaidi duniani huko Manaus mjini Amazon.

Mnara huo kwa jina Amazon observation Tower, unatazamiwa kutumika katika utafiti wa mapana wa hali ya anga.

Utakuwa na vifaa maalum venye uwezo mkubwa wa kukusanya data kuhusu gesi chafu iliyo hewani, chembe chembe za erosoli na hali ya anga ya kila uchao katika msitu wa Amazon.

Eneo hilo la Amazon ndilo linalinaloshuhudia mvua kubwa zaidi kila msimu.

Wanasayansi wa Brazil na Ujerumani wanatumai kuutumia mnara huu katika uchunguzi wao wa vyanzo vya gesi chafu na mabadiliko ya hali ya anga.

Kutokana urefu wake, mnara huu utawezesha wanasayansi kuelewa mabadiliko ya mwelekeo wa upepo kwa kitalifa cha zaidi ya kilomita mia moja katika msitu wa Amazon.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msitu wa Amazon umekuwa ukikatwa kwa muda

Msitu wa Amazon ni kati ya misitu mikubwa zaidi duniani inayoathiri mazingira kwani inahusika pakubwa katika kuongeza na kupunguza kiwango cha hewa aina ya (carbon) angani.

Kulingana na bw. Paulo Artaxo, mwelekezi wa mradi huo kutoka chuo kikuu cha Sao Paulo, amesema mnara huo utasaidia pakubwa katika juhudi za kutafuta majibu ya maswali mengi kuhusu mabadiliko ya hali ya anga duniani.

Aidha, mnara huu unatarajiwa kutumiwa pamoja na minara mingine midogo ambayo tayari imejengwa nchini humo.

Kulingana na wajenzi, mnara huu utafanana na ule uliojengwa Siberiaya kati katika mwaka wa 2006.