Social Democrats kuunda Serikali Sweden

Haki miliki ya picha AP
Image caption Social Democrats kuunda Serikali mpya Sweden

Kiongozi wa chama cha Sweden cha Social Democrats anatazamiwa kuunda Serikali ya mrengo wa Kati baada ya Waziri Mkuu Fredrik Reinfedt kukubali kushindwa katika Uchaguzi mkuu jumapili.

Hata hivyo chama cha mrengo wa kulia kinachopinga watu kuhamia nchini humo kiliongeza viti mara mbili Bungeni na kuwa chama cha tatu kwa ukubwa.

Haki miliki ya picha .
Image caption Raiya Sweden wakishangilia kushinda Uchaguzi

Muungano wa vyama vya mrengo wa Kati inayojumuisha Social Democrats, the Greens na Left Party walishinda na asilimia 43.6 % ya kura, lakini chama kinachotawala cha Alliance kilishindwa kwa asilimia 10% na kuwa na kura asimilia 40% wakati wa mwisho wa kuhesabu kura.

Waziri Mkuu anayeondoka Fredrik Reinfeldt aliwashukuru wafuasi wake kwa imani waliyokuwa nayo kwake kwa miaka minane aliyotawala, kabla ya kukubali kushindwa na kustaafu kama kiongozi wa chama chake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa waziri mkuu wa Sweden amekubali kushindwa katika Uchaguzi

Kiongozi wa Social Democrat Stefan Lofven sasa anatarajiwa kuunda Serikali ya mseto, ingawa hatapata Wabunge wa kutosha kupitisha sheria yoyote bila kushauriana na upinzani.

Chama kinachopinga watu kuhamia nchini humo kilishinda asilimia 13%ya kura zote.

Hii inamaanisha kuwa Chama hicho kitakuwa cha tatu kwa ukubwa na kitakuwa na uwezo wa kuhakikisha kuwa hakuna mswada unaopitishwa bila kushiriki kwake.