Ufaransa na Iraq wakutana

Haki miliki ya picha Getty
Image caption John Kerry akiwa na viongozi wa Kiarab

Nchi za Ufaransa na Iraq leo wanakutana na kufanya mkutano wa kimataifa mjini Paris ili kukubaliana kwa pamoja,na pia kuweka mikakati ya kulitokomeza kundi la wanamgambo wa dola ya kiislam.

Waziri wa mambo ya kigeni nchini Marekani John Kerry ameeleza kua ameweza kuungananisha takribani nchi arobaini na zote zimekubali kuingia kwenye muunganohuo zikiwemo nchi za Kiarab kulikabili kundi hilo nchini Iraq na Syria.

Ushiriki wa nchi za kiarabu katika mkakati huo kunaongeza nguvu na matumaini ya kupata ushindi wa kampeni hiyo.wakati huo huo baraza la usalama la umoja wa matifa umelaani vikali mauaji ya mateka wa kiingereza David Haines aliyechinjwa na kundi hilo la dola ya kiislam na kuliita tukio hilo kua ni la kuchukiza na la kikatili mno.

Uingereza mpaka kufikia sasa imechukua jukumu la kupambana na kundi hilo angani, na Waziri Kerry amethibitisha kua nchi za kiarab nazo zimethibitisha kujiunga kwenye mashambulizi ya angani.