Wapiganaji washambulia chuo Nigeria

Image caption Kundi la Boko Haram limekuwa kero kubwa kwa wananchi wa Nigeria ila washambuliaji wa sasa haijulikani ikiwa ni Boko Haram

Duru kutoka Kaskazini mwa Nigeria zinasema kuwa watu waliojihami wamevamia chuo cha mafunzo ya Ualimu katika kijiji cha Kano.

Mwanafunzi mmoja aliyeshuhudia tukio hilo amesema kuwa amehesabu maiti kumi na saba katika tukio hilo.

Watu hao wanasemekana kufyatua risasi na kulipua maguruneti huku wanafunzi wakikimbilia maisha yao.

Huku hayo yakijiri mamlaka nchini humo imethibitisha kuwa miili ya watu sabini imeokolewa kutoka vifusi vya jengo moja la kanisa lililoporomoka huko Lagos siku ya Ijumaa.

Mamlaka ya usimamizi wa majanga ya dharura imesema kuwa watu mia moja na thelathini wamenusuriwa.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema kuwa raia 67 wa Afrika kusini wamefariki na wengine kadhaa kujeruhuwa katika mkasa huo.

Rais Zuma ameongeza kusema kuwa hilo ndilo janga la hivi punde kubwa zaidi la kigeni kusababisha vifo vya raia wake wengi kwa kipindi kimoja.