Scotland kuamua ikiwa itajitenga au la

Image caption Wanaopigia debe Scotland kujitenga

Wanasiasa wanaendelea na shughuli za kampeni hii leo, ikiwa siku ya mwisho kabla ya kupiga kura ya maamuzi nchini Scotland.

Mnamo siku ya Alhamisi Scotland itapiga kura ya maoni kuamua iwapo itaendelea kuwa katika muungano na Uingereza au la.

Pande zote mbili za kisiasa zimekuwa zikitoa maombi ya mwisho kwa wapiga kura.

Kiongozi wa kundi linalotaka Scotland kujitenga, Alex Salmond, amewaomba raia wajichukulie wajibu huu muhimu mikononi mwao.

Image caption Wanaopinga Scotland kujitenga

Naye Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown amewaonya wakaazi wa Scotland kuwa wasithubutu kufutilia mbali muungano wenye faida kubwa wa muda mrefu.

Ushindani umekuwa mkali ingawa matokeo ya kura ya maoni yaliyotolewa na mashirika matatu ya kujitegemea yanaonyesha kuwa wale wanaotaka Scotland iendelee kuwa sehemu ya Uingereza wanaongoza na pinti nukta nne pekee.