Paundi mjadala kujitenga Scotland

Haki miliki ya picha AFP

Huku raia wa Scotland wakitarajia kupiga kura ya maoni hapo kesho sarafu ya Paundi ni mojawapo ya masuala ambayo yamekuwa yakizungumzwa kwenye kampeni ambapo serikali kuu imewaambia waskochi kwamba hawatatumia sarafu hiyo ikiwa watajitenga.

Wakati huo huo Kiongozi wa chama cha Scotish National Party, Alex Salmond, ametoa wito kwa wapiga kura kuhakikisha kuwa nafasi ya kuunda Scotland huru haiwaponyoki mikononi mwao.

Kura za maoni zilizofanywa na mashirika mbalimbali kutangulia upigaji kura zinaonyesha kuwa wanaotaka Scotland kuendelea kuwa sehemu ya Uingereza wanaongoza kwa nukta nne pekee.