Ebola:Wahudumu wengine washambuliwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wadadisi wanasema nchi nyingi za Magharibi mwa Afrika zinakabiliwa na changamoto za miundo msingi

Shirikisho la kimataifa la msalaba mwekundu, limesema kuwa kikundi kingine cha wahudumu wa afya kilishambuliwa Jumanne Kusini Mashariki mwa Guinea walipokuwa wanakusanya miili ya watu waliofariki kutokana na Ebola.

Mfanyakazi mmoja wa shirika hilo, anauguza majeraha baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo katika eneo la Forecariah.

Kulingana na mkazi mmoja, jamaa wa wagonjwa waliofariiki walianza kuwashambulia wafanyakazi hao sita wa kujitolea , na kuharibu magari yao pamoja na kuwashambulia kwa mawe wafanyakazi hao.

Huu ni uvamizi wa hivi karibuni dhidi ya wahudumu wa afya ambao bila shaka unatatiza juhudi za kupambana na ugonjwa huo mkali.

Wiki jana madaktari wengine na wandishi wa habari walishambuliwa Magharibi mwa nchi hiyo.