Cyprus kuwaokoa watu 300 kutoka baharini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mamia ya wakimbizi wamekuwa wakifunga safari kutoka Afrika wakiabiri vyombo hafifu mno

Serikali ya Cyprus imetangaza kuwa imeanzisha operesheni ya a kuwaokoa watu 300, wanaodhaniwa kuwa wakimbizi kutoka Syria, waliokwama mwa Kisiwa hicho.

Mashua za kushika doria na meli zimetumwa katika eneo hilo, huku kukiwa na hofu kuwa huenda chombo hicho kinaelekea kuzama.

Walionekana maili 55 baharini sawa na kilomita mia moja kusini mwa mji wa mapumziko wa Paphos.

Helikopta ziko katika eneo la tukio hilo.

Wizara ya Ulinzi ya Cyprus imesema kuwa inadhani watu wote waliokwama katika chombo hicho ni wanawake na watoto, wengi wao wakiwa wakimbizi kutoka Syria.

Taarifa hiyo ya Wizara inasema kuwa shughuli hiyo ya uokoaji ilianzishwa baada ya mawasiliano ya radio kutoka kwa chombo hicho, kinachowabeba wakimbizi hao, kusema kuwa wako taabani.

Kuna hofu kuwa huenda kikazama wakati wo wote.

Hali ya hewa ni mbovu sana katika eneo hilo Kusini Magharibi mwa mji ya Paphos.

Image caption Cyprus imeanzisha operesheni ya kuwaokoa watu 300 kutoka Baharini

Kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wakimbizi wanaovuka Bahari ya Mediterranean mwaka huu, wengine wao wakitoroka vita huko Syria.

Safari nyingi za wakimbizi zimekuwa zikifanywa katika hali ya habari, mashua zilizojaa watu kuliko kiasi, na zilizozeeka sana.

Mapema mwezi huu, Wakimbizi kutoka Palestina walisema kuwa mamia ya abiria waliokuwa wakisafiri nao katika mashua walikufa maji baada ya mashua hiyo kuharibiwa makusudi na walanguzi wa kuwasafirisha watu waliokuwa wakitaka kuwahamishia katika mashua ndogo zaidi.