Ahukumiwa kifo Kenya kwa kuavya mimba

Haki miliki ya picha PA
Image caption Mahakama moja nchini Kenya imemhukumu muuguzi mmoja kunyongwa kwa kuavya mimba.

Mwuguzi mmoja nchini Kenya amehukumiwa kifo baada ya mwanamke aliyemsaidia kuavya mimbia kufariki miaka mitano iliyopita.

Nchini Kenya kuavya mimba ni kinyume cha sheria ingawa matabibu kadhaa huendesha shughuli hizo kisiri kwa sababu mapato yake ni makubwa.

Jackson Namunya Tali, mwenye umri wa miaka 41, amehukumiwa kifo na Jaji Nicholas Ombija mjini Nairobi, baada ya kupatikana na kosa la kusababisha kifo cha msichana Christine Atieno katika kituo cha afya anachosimamia .

Kulingana na taarifa ya mashahidi, Msichana Atieno alitunga mimba ambayo hakutarajia na mnamo Julai , mwaka 2009, na kuamua kutafuta msaada kwa Tali katika kituo chake cha afya katika eneo la Gachie, viungani mwa jiji la Nairobi ambapo alitaka kuavya mimba hio.

Jaji aliambiwa Kwamba licha ya jaribio la kuitoa mimba hiyo haikutoka na badala yake mtoto aliyekua tumboni alikufa, hali iliyosababisha marehemu kuvuja damu nyingi.

Mshtakiwa alipogundua hali ilikua mbaya alianza kumpa msichana huyo madawa za maumivu.

Kisha akampeleka katika hospitali ndogo ya Kaunti ya Kiambu.

Haki miliki ya picha other
Image caption Jaji alimpata na hatia ya kusababisha kifo cha mama na mtoto

Wahudumu wa afya katika hospitali ya Kiambu walipendekeza mgonjwa kupelekwa kwa matibabu maaluum katika hospitali ya nyingine ambapo angepokea matibabu ya dharura kwani hali yake ilikua mbaya.

Hata hivyo msichana huyo, ambaye wakati huu wote alikuwa akivuja damu akiwa ndani ya gari la mshtakiwa alifariki dunia na muuguzi aliyemhudumiwa kulaumiwa kwa kifo hicho na kushtakiwa.

Hii ndio hukumu kali zaidi kutolewa nchini Kenya kuhusiana na kifo kutokana na kuavya mimba.

Nchini Kenya kutoa haikubaliwi ila ikiwa maisha ya mama yako hatarini

Mjadala ya kuhalalisha uavyaji mimba umevutia hisia kali nchini Kenya wanaounga wakisema itasaidia afya ya uzazi huku wapinzani wakisema ni mauaji ya kiumbe asiye na hatia.