Watu 18 wauawa kwa mashambulizi Nigeria

Image caption Wanamgambo wa Boko Haram

Takriban watu 18 wameuawa na watu wanaoshutumiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram mjini Shaffa, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Shuhuda wa tukio hilo amesema mashambulizi hayo yalifanyika siku ya jumatano jioni na kuendelea mpaka alhamisi asubuhi.

Wanamgambo wa kiislamu wamesema wameharibu makanisa kadhaa na makazi mjini humo, na kushambulia kijiji.

Mji wa Shaffa uko kwenye jimbo la Borno,jimbo ambalo limeathiriwa na mashambulizi ya wanamgambo.