Taleban yateka mji wa Ghazni Afghanistan

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Afisa wa usalama akishika doria katika mji wa Ghazni

Maafisa huko mashariki mwa Afghanistan wanasema kuwa wapiganaji wa Taliban wamechukua udhibiti wa baadhi ya Wilaya katika jimbo la Ghazni.

Watu zaidi ya 70 wanahofiwa kufariki katika Wilaya ya Ajrestan katika mapambano hayo ya kuteka vijiji vyao hapo jana jioni.

Ripoti zinasema Kuna makabiliano makali ya risasi huku walinda usalama wakifanya kila wawezalo kujaribu kutwaa tena wilaya hizo zilizotekwa.

Ghazni ni mji muhimu umnaochukuliwa kama mlango unaounganisha mji mkuu Kabul na eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Wadadisi wa hali ya usalama nchini humo wanasema kuwa kutekwa kwa mji huo ni ilani kwa miji iliyoko karibu na

Ghazni huenda pia zikatekwa.