Dreamliner yatua Glasgow kwa dharura

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Dege la kisasa Dreamliner lot aina ya boing

Ndege kubwa naya kisasa maarufu kama Dreamliner ikiwa na abiria 260 ndaniye imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Glasgow,nchini Scotland.

Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Polish airline Lot ,ilikua inafanya safari yake kutoka Chicago kuelekea Warsaw ilipotangaza dharura kuwa katika hali ya dharura.

Na mara baada ya kutua abiria waliondolewa uwanjani hapo, na ndege kufanyiwa uchunguzi wa kilichosababisha itue kwa dharura ingawa mpaka sasa chanzo cha dharura hiyo hakijajulikana.

Nao uwanja wa ndege wa Glasgow uliendelea na shughuli zake kama kawaida na ndege hiyo haikuleta usumbufu wowote.

Ingawa taarifa za awali zinaonyesha kuwa ndani ya ndege hiyo kulikua na harufu ya moshi, na baadaye uchunguzi ulipofanywa ulionyesha kua hakukuwa na chanzo cha moto kilichosababisha harufu hiyo ya moshi.