Hungary yasitisha gesi Ukraine

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nishati ya gesi na njia zake

Kampuni kutoka Hungary inayoshughulikia usambazaji gesi ya FGSZ, imetoa tamko kua imesitisha upelekaji wa gesi kwa nchi jirani ya Ukraine bila kikomo.

Kwa kawaida Ukraine ilikua ikipokea gesi kutoka katika nchi za Hungary, Poland na Slovakia nah ii ni baada ya Urusi kusitisha pia zoezi kama hilo kuelekea Ukraine mwezi june kutokana kutolipwa kwa bill.

Kampuni kubwa la usambazaji wa gesi kutoka Ukraine la Naftogaz imethibitisha usitishwaji huo na kuelezea uamuzi huo kua haukutegemewa na usioelezeka.kampuni hiyo pia imeeleza kua imesitisha upelekaji wa gesi nchini Ukraine ili kutoa fursa kwa ukuzaji na usamabazaji wa bidhaa hiyo nchini Hungary.

Wakati huu ambapo majiraya baridi yanakaribia kuna hofu kuwa huenda Ukraine haitaweza kuwahudumia watu majumbani na kampuni za usambazaji umeme hazitaweza kujiendesha bila ya kupata gesi kutoka Urusi.

Mawaziri wa nishati wa Urusi na Ukraine wanakutana mjini Berlin katika mkutano unaounganisha umoja wa ulaya kwa lengo la kutaka kutafuta suluhu la marufuku hiyo.

Hungary imetoa ,maelezo yake kuwa usitishwaji huo umetokea kwa sababu za kiufundi na ni kwasababu ilikua inajua wazi yakuwa mahitaji makubwa ya usafirishaji wa gesi yataongezeka.

Haya yote yanatokea siku tatu baada ya mkutano uliofanyika huko Budapest kati ya viongozi wa kampuni kubwa la usambazaji wa gesi ya Gazprom na waziri mkuu wa Hungary ,Viktor Orban.

Waziri Orban amekua mpinzani wa hatua zilizochukuliwa na umoja wa ulaya na ameanzisha uhusiano mpya na Moscow kuliko hata nchi jirani za Magharibi zilizomo katika umoja wa ulaya .

Mapema mwaka huu kampuni hilo kubwa la usambazaji gesi Gazprom na Rais wa Urusi Vladimir Putin walionya hatua za umoja wa ulaya endapo wataendelea kupeleka gesi huko Ukraine.