Chuo cha kidini chafungwa Kenya

Image caption Madrasa ya Ngulini iliyofungwa kwa madai kuwa inafunza itikadi kali za kidini

Maafisa nchini Kenya wameifunga Madrassa au shule ya maunzo ya dini nchini humo kwa madai kuwa inafunza masomo ya itikadi kali.

Madrassa hiyo iliyo mjini Machakos, Mashariki mwa Nairobi, imechukuliwa hatua hiyo baada ya vijana kadhaa waliokuwa wakihojiwa na polisi kuitaja.

Vijana hao wanazuiliwa kwa tuhuma za kuhusiana na wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia.

Kundi la Al-Shabab limekuwa likifanya mashambulio kadhaa nchini Kenya kama hatua ya kulipiza kisasi kuwepo wanajeshi wa nchini hiyo Somalia.