Simu kutumika angani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Je zitaruhusiwa angani

Shirika la usalama angani la umoja wa ulaya (EASA) limesema vifaa vya kielekroniki vinaweza kutumika pindi ndege iwapo angani kama zinzvyotumika simu za viganjani wakati wa safari.

Na shirika hilo la EASA limesema kwamba vifaa vya kielekroniki havina athari yoyote kiusalama.

Tangazo hili linawaweka kwenye nafasi nyingine wenye kuongoza ndege na wafanyakazi wake kuwaruhusu abiria kutumia simu zao za viganjani baada ya kujihakikishia usalama baada wakijiridhisha.

Kwasasa abiria wasafirio kwa njia ya anga wanapaswa kuzima simu zao za viganjani ama kuweka katika njia ya flight mode ama kuruhusiwa kupiga simu katika viwanja vya ndege.

Shirika hilo linasema kwamba kila shirika la ndege yatapaswa kufanya uchunguzi wao ili kuona mifumo ya ndege haiathiriwi na muingiliano wa vifaa hivyo vya kielekroniki na siginal zake kabla hawajaweka sheria zao katika utendaji kazi.

Shirika la EASA linaandaa utaratibu kwa mashirika ya ndege kufanya maamuzi ya usalama.