Kesi ya Mubarak yaahirishwa nchini Misri

Image caption Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak akiwa mahakani

Uamuzi wa kesi inayomkabili rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak kuhusu mashtaka ya ufisadi na mauaji ya waandamanaji wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 umeahirishwa.

Jaji alisema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na sahabu ya kuwepo kwa ushahidi ambao bado mahakama haijausikiliza.

Wakati wa kesi ya leo kanda moja ya video ilionyesha mrundiko wa stakabadhi za ushahidi.

Bwana Mubarak alipatikana na hatia mnamo mwaka 2012 na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini baadaye hukumu hiyo ikabatilishwa.

Mahakama hiyo imesema kuwa itatoa hukumu yake mwezi Novemba.