Hong Kong:Waandamana kuipinga Uchina

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waandamanaji Hong Kong

Maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono demokrasi mjini Hong Kong wameanza kampeni ya kukwamisha shughuli katika maeneo ya kati kati ya mji.

Vugu vugu linalojulikana kama occupy Central lilichochewa na mandamano ya wanafunzi waliovamia makao makuu ya serikali ijumaa usiku na kusababisha makabiliano na polisi.

Waandamanaji hao wanaitaka Uchina kuwapa uhuru kumchagua kiongozi wa mji wa Hong Kong mwaka 2017.

Waandamanaji wana hasira kuwa Uchina inataka wagombea wanaogemea upande wake kusimama uchaguzi.