Braulio Zaragoza auawa Mexico

Haki miliki ya picha Milenio
Image caption Mgahawa pwani ya Acapulco

Kiongozi wa kisiasa nchini Mexico,Braulio Zaragoza, ameauwa kwa risasi katika mgahawa wa hoteli Magharibi mwa mji wa Acapulco.

Mwendesha mashtaka ameeleza kua Bwana Zaragoza alikuwa kwenye mkutano pamoja na wanasiasa wengine mapema jana wakati ambapo watu watatu waliokuwa na bunduki walipomfuata mezani na kummiminia risasi mara kadhaa kwa nyuma.

Bwana Zaragoza alikua ni kiongozi wa upinzani mwenye msiamo mkali wa chama cha National Action Party ambacho makao yake makuu yako katika viunga vya mji wa Guerrero.

Polisi wametoa taarifa yakwamba chanzo cha kifo cha Zaragoza hakijafahamika na wameeleza tu kua wanasiasa wenye msimamo mkali na wanaharakati wanalengwa mno miaka ya hivi karibuni na wauza mihadarati wakubwa na hasa pwani ya Mexico.