Je vifo vya watoto vimepungua Afrika?

Hapo septemba mwaka wa 2000, viongozi kutoka kote duniani walitia saini mkataba wa kutiumiza Malengo nane ya kimaendeleo ya Milenia (Millennium Development Goals (MDG)).

Kila lengo likidhamiria kuboresha maisha ya watoto wachanga kote ulimwenguni hasa kiafya, kielimu na hata katika kutoa nafasi za kujiendeleza.

Lengo muhimu zaidi kati ya haya ikiwa ni lile la kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaoaga dunia kabla ya kufikisha miaka mitano.

Mahimbo Mdoe kutoka shirika la kushughulikia watoto (Unicef) lililo chini ya umoja wa mataifa, anaelezea jinsi mataifa yanavyokazana kutatua tatizo hili na jinsi taifa la Malawi linavyozidi kufanikiwa katika juhudi zake za kutimiza lengo hili.

Hatua kadhaa zimechukuliwa lakini bado kunaendelea kushuhudiwa vifo vinavyoweza kuzuiliwa.

Kwa mujibu wa Unicef, mafanikio yanaendelea kupatikana katika juhudi za kupunguza vifo vya watoto wachanga, kwani kwa sasa idadi ya vifo vya watoto inaendelea kupungua kwa kasi ya juu zaidi kuliko karne nyingine Hata hivyo, watoto zaidi ya milioni 6 hufa kabla ya kufikisha miaka mitano hususan kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika.

Mataifa ya Afrika yaliyo kusini mwa jangwa la Sahara ndiyo yaliyo na asilimia kubwa ya vifo ya watoto wachanga wenye umri ulio chini ya miaka mitano.

Tangu 1990,MDG imekuwa ikilenga kupunguza vifo hivyo kwa thuluthi mbili 2/3 kufikia mwisho wa mwaka 2015. Nchi ya Malawi ni kati ya mataifa machache kutoka ukanda huu kutimiza lengo hili.

Wakati hatari zaidi

Majuma manne ya kwanza tangu kuzaliwa kwa mtoto na hasa masaa ya kwanza duniani ndiyo hatari zaidi. Ingawa idadi ya watoto wanaokufa katika muda huo imepungua, kasi yake imekuwa ndogo sana. Katika mwaka wa 2003, watoto milioni 2.8 walikufa katika muda wa siku 28 toka kuzaliwa.

Image caption Mtarajio ifikapo mwaka wa 2015

Lini lengo la Umoja Wa Mataifa litatimizwa?

Kati ya mwaka wa 1990 na 2003 watoto milioni 223 kutoka kote ulimwenguni walikufa kabla ya kutimiza miaka mitano. Idadi hii ni kubwa sana hata kuliko hata idadi ya watu wote walio nchini Brazil. Kwa mwendo huu, lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa thuluthi mbili 2/3 halitotimizwa kabla ya mwaka 2026.

Image caption Magonjwa mengine yanayosababisha vifo vya watoto wachanga.