Sheria yawalinda wanafunzi kingono US

Haki miliki ya picha AP
Image caption Gavana Jerry Brown anasema lazima mwanafunzi aridhie kufanya mapenzi akiwa katika hali yake sawa kiakili

Jimbo la Carlifonia nchini Marekani, limekuwa jimbo la kwanza nchini humo kuwataka wanafunzi wa masomo ya juu wanaofadhiliwa na serikali kuelewa kwamba lazima waridhie wenyewe kabla ya kujihusisha na vitendo vya ngono.

Sheria hiyo iliyotiwa saini na gavana wa jimbo hilo,Jerry Brown -inafafanua sharti la kuridhia kabla ya kujihusisha kingono kama makubaliano ya hiari. ''Ikiwa msichana atakosa kujibu ombi la ngono haimaanishi kuwa ameridhia,'' alisema gavana wa jimbo hilo.

Chini ya sheria hiyo yeyote ambaye ni mlevi au ametumia dawa za kulevya , hana fahamu au amelalal hawezi kuridhia kufanya ngono, kwani hayuko katika hali yake ya kawaida kiakili. .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sheria hii inanuia kuwalinda wanafunzi wa vyuo vikuu.

Wabunge wanasema kuwa ridhaa ya kufanya tendo la ndoa sio lazima iwe kukubali kwa kinywa bali pia kwa njia nyingine yoyote ambayo haionyeshi kuwa mwanafunzi amelazimishwa.

Wanaharakati wanaounga mkono sheria hiyo mpya wanasema itabadili dhana iliyopo kuhusu kitendo cha ubakaji

Rais Barack Obama alizindua mpango sawia na huo mapema mwaka huu akilenga kukabiliana na visa vya udhalilishaji wa kimapenzi kwa wanafunzi wa vyuo na taasisi za masomo ya juu.