Ebola na mateso ya Watoto,A.Magharibi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ebola

Umoja wa mataifa umesema takriban watoto 3,700 katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone wamepoteza wazazi wao kutokana na ugonjwa wa Ebola hali inayowafanya kuishi maisha ya ukiwa na kukosa msaada wa kimaisha hali ambayo shirika la kuhudumia watoto duniani Unicef wanasema msaada wa haraka unahitajika.

Hata hivyo pia ripoti hiyo inahimiza hatua za haraka kama vile kuwafariji watoto hao kuchukuliwa.

Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kuwa zaidi ya watu 3,000 wamekufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi na kusababisha idadi kubwa ya watoto kukosa wazazi wao.

Watoto waliokutwa pekee yao maeneo ya hospitali walikofia wazazi wao hawana kwa kwenda huku wengine waliobahatika wamefanikiwa kurejea katika makazi yao bila kuwa na msaada wowote wa kuhudumiwa na majirani zao.

Hivyo kutokana na mazingira magumu kama hayo ya watoto hao umoja wa mataifa umehimiza hatua za haraka kuchukuliwa.