Waombwa kukoma kuandamana Hong.K

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption Kiongozi wa Hong Kong amesema kuwa Uchina haitabadilisha kanuni za uchaguzi

Kiongozi wa jiji la Hong Kong C Y Leung ametoa wito wa kusitishwa maandamano ambayo amesema yamedumaza shughuli katika jiji zima.

Amesema kuwa maandamano hayo hayawezi kubadil msimamo wa China juu ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Haki miliki ya picha AFP Getty Images
Image caption Raiya wa HK wakiwasha taa za simu zao usiku

Bwana Leung pia amekataa kuitikia wito wa kujiuzulu kwak ekutoka kwa vuguvugu lililopanga maandamano hayo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raiya wamekataa kuondoka mabarabarani wakitaka madiliko katika sera za uchaguzi

Wakati huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka utawala kuchukua hatua.

Katika mkutano wa wanahabari msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono matakwa ya watu wa Hong Kong.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia wa Hong Kong wakivurumushiwa moshi

Makumi kwa mamia ya waandamanaji wa Hong Kong wanaendelea na maandamano yao kwa siku nyingine tena baada ya kudhoofisha maeneo muhimu ya jiji hilo wakati wa mchana.

Image caption Maandamano hayo yamebandikwa jina maandamano ya miavuli.

Waandamanaji hao sasa wanamtaka Mkuu wa utawala wa Hong Kong Leung Chun-Ying ajiuzulu..

Wakati huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka utawala kuchukua hatua.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raiya wa Hong Kong akijiandaa kwa makabiliano na polisi

Katika mkutano wa wanahabari msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono matakwa ya watu wa Hong Kong.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamani wamebandika karatasi zenye ujumbe kwenye mabasi ya umma HK

"Duniani kote, na hii ni kweli katika Hong Kong na maeneo mengine, Marekani inaunga mkono kimataifa, uhuru, kama vile uhuru wa kukutana kwa amani na uhuru wa kujieleza.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Maelfu ya waandamanaji katika barabara za Hong kong

Marekani inautaka utawala wa Hong Kong kuchukua hatua, na kwa upande wa waandamanaji kutoa maoni yao kwa amani"