Johannesburg ina panya hatari

Image caption Panya wala watoto

Mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini ni mmoja wa miji inayokua kwa kasi barani Afrika, lakini mji huo unakabiliwa na tatizo la kuvamiwa na panya walionona ambao huwatafuna watoto wadogo majumbani na wengine kufariki dunia. Maafisa wa halmashauri ya jiji la Johannesburg sasa wamezidisha juhudi ya kupambana na tatizo hilo ambalo limekuwepo kwa muda mrefu.