Julius Malema mahakamani leo

Image caption Julius Malema

Hii leo Julius Malema kiongozi wa chama cha Economic Freedom Front (EFF) nchini A-Kusini atafika mbele ya Mahakama kuu ya Polokwane mkoa wa Limpopo kujibu mashitaka ya rushwa na ufisadi yanayomkabili .

Malema anashitakiwa pia na wenziwe watatu,ambao kwa pamoja wanakabiliwa na makosa ya kuhaulisha pesa katika Kampuni mmoja inayodaiwa kuwa ni ya Julius Malema .