Nick Minaj mc wa MTV

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nicki Minaj

Mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka Nicki Minaj anaelekea kukamata mic maaruku kama mc katika tuzo za mwaka huu za MTV Europe Music Awards maarufu kama EMAs mjini Glasgow, nchini Scotland. Kama hiyo haitoshi mlimbwende huyo atatumbuiza kwenye tamasha hilo la ugawaji tuzo November 9.

Mpaka sasa mwanadada Katy Perry anaongoza kwa kuchaguliwa kuwania tuzo takriban saba ikiwemo ile ya best female, pop act, video na maonesho hai.

Katty anachuana na mwanadada mwingine Ariana Grande, ambaye anawania tuzo sita wakati huo huo 5 Seconds of Summer na Pharrell Williams wanawania tuzo tano kila mmoja wakiwatangulia One Direction.

Nicki Minaj alitumbuiza wimbo wake wa Anaconda katika tuzo za MTV VMA mjini California mwezi August mwaka huu anawania tuzo zingine nne katika tuzo za EMAs.