Bingwa wa Berlin Marathon asherehekewa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bingwa wa Berlin Marathon Dennis Kimetto

Mwanariadha Dennis Kimetto amepata makaribisho ya kufana aliporudi nchini Kenya siku ya jumapili,baada ya kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za Marathon za mjini Berlin.

Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye alianza mbio za kulipwa miaka mitano iliopita amesema kuwa hakutarajia kuvunja rekodi ya dunia.

Alimpita mwenzake wa Kenya Emmanuel Mutahi ikiwa imesalia chini ya maili tatu ili kuweka rekodi mpya ya masaa mawili dakika mbili na sekunde hamsini na saba.

Kimetto alikabidhiwa maua na kuzungushwa katika mji mkuu wa Nairobi.

Alisema ''Nilienda Berlin ili kushindana lakini namshkuru mungu kwamba nimerudi nyumbani nikiwa bingwa wa dunia,nilishangaa.

Rekodi ya awali iliwekwa katika eneo hilo hilo miezi kumi na mbili iliopita na mwanariadha mwengine wa Kenya Wilson Kipsang,aliyekimbia masaa mawili dakika tatu na sekunde ishirini na tatu.